Makubaliano ya amani nchini Sudan Kusini Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amelivunja bunge lake na kuunda serikali ya umoja, katika har...
| Makubaliano ya amani nchini Sudan Kusini |
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir
amelivunja bunge lake na kuunda serikali ya umoja, katika harakati za
kupiga jeki makubaliano ya amani yanayolenga kumaliza vita vya wenyewe
kwa wenyewe vya takriban miaka miwili.
Thuluthi moja ya mawaziri wa bunge hilo jipya ni wanachama wa chama cha SPLM-IO kilichobuniwa na aliyekuwa kiongozi wa waasi Riek Machar,ambaye alirudi mjini Juba mapema wiki hii ili kuapishwa kuwa makamu wa kwanza wa rais.
Makumi ya maelfu wameuawa na watu milioni 2 wakiwachwa bila makao katika mgogoro huo wa Sudan Kusini ambayo ilipata uhuru wake mwaka 2011.
Mwandani wa rais Salva Kiir Kuol Manyang atasalia kuwa waziri wa Ulinzi na David Deng Athorbei akiwa waziri wa fedha ambao watajaribu kuimarisha uchumi ulioathiriwa na vita vya zaidi ya miaka miwili.
Wizara muhimu ya mafuta ilipewa Dak Duop Bichok.
| Riek Machar na Salva Kiir |
Alor alikuwa mwanachama wa kundi linalojiita ''wafungwa wa zamani'',viongozi wenye ushawishi waliokamatwa wakati vita vilipoanza,lakini baadaye wakaachiliwa baada ya shinikizo kali.
Kiongozi wa upinzani na mkosoaji mkubwa Lam Akol atakuwa waziri wa kilimo na usalama wa chakula,ikiwa ni wizara muhimu ambapo watu milioni tano wanahitaji msaada,huku maeneo mengine yakikabiliwa na ukame.



