mkuu wa mkoa wa Simiyu, Antny Mtaka MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka amewaonya maofisa wa polisi wanaojihusisha na tabia ya kuwabam...
![]() |
| mkuu wa mkoa wa Simiyu, Antny Mtaka |
Amesema polisi wa aina hiyo hawafai kuendelea kulitumikia jeshi hilo, kwani wanalifedhehesha. Alitoa onyo hilo jana wakati akizungumza na askari hao wenye vyeo mbalimbali mjini Bariadi. Aliwataka askari wabadilike kifikra na kuongeza ufanisi katika maeneo yao ya kazi.
“Haiwezekani tukaendelea kuwa na askari polisi ambaye amekuwa akiwabambikia kesi wananchi kwa lengo la kutaka kupata pesa na wengine mnapopanga kwenda kukamata wahalifu wao wanawapatia taarifa…,” alisema.
Alisema maofisa na wakaguzi wa polisi wana wajibu wa kuimarisha usimamizi wa nidhamu na maadili kwa askari polisi, fedha, vitendea kazi pamoja na miundombinu ya jeshi hilo.
Naye Kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu, Onesmo Lyanga amewaonya askari wa jeshi hilo mkoani humo wasiozingatia maadili na miongozo ya jeshi hilo pamoja na sheria za nchi watafukuzwa kazi mara moja.
“Mkuu wa mkoa mimi niko timamu nitahakikisha ya kuwa kauli mbiu ya Serikali ya wamu ya tano ya Hapa Kazi Tu inatekelezwa ndani ya jeshi la polisi mkoa wa Simiyu na wale askari 10 ambao nawafahamu kwa majina walioonesha utovu wa nidhamu mbele yako kwenye sherehe nitashughulika nao,”alisema.




