mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Michael Lekuler MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Arusha, Michael Lekule Laizer amemuony...
![]() |
| mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Michael Lekuler |
Baadhi ya hujuma hizo zinazodaiwa kufanywa na halmashauri hiyo inayoongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ni pamoja na kuzinyima miradi kata zinazoongozwa na madiwani wa CCM.
Laizer ametoa tahadhari hiyo mjini hapa jana katika kata ya Mangola Barazani alipokuwa akizungumza katika mkutano wa ndani na viongozi wa chama wa ngazi za matawi na kata kuhusu kero mbalimbali za wananchi wa kata hiyo.
Mwenyekiti huyo alifikia hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa diwani wa kata hiyo kupitia CCM, Lazaro Emanuel.
Emanuel alisema kwa kipindi kirefu tangu ameingia madarakani amekuwa akikosa ushirikiano kutoka kwa uongozi wa halmashauri hiyo akiwepo pia mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Mabula na hadi sasa hajakubaliwa ombi la mradi hata mmoja.
Alisema hali hiyo haijaishia kwake tu bali kwa madiwani wengine wa CCM kutoka kata zingine ambapo pia wamekuwa wakitengwa katika baadhi ya vikao hususan vya kuandaa bajeti ya halmashauri hiyo na madiwani wa Chadema wamekuwa wakiitana katika vikao vichochoroni na kuandaa bajeti kisha wao hutaarifiwa ikiwa imeshafikishwa hazina.
Alisema hata bajeti iliyopelekwa hivi karibuni hazina wao kama madiwani wa CCM hawakuifahamu wala kushirikishwa mapema bali wamekuja kuambiwa waijadili wiki tatu tangu kufikishwa hazina ilipoandaliwa na madiwani wa Chadema pekee na mkurugenzi huyo, jambo lililowasababisha madiwani hao kususia baraza hilo na kutoka nje ya kikao.
Akijibu hayo, Laizer alimtaka diwani huyo kuitisha mikutano ya wananchi wake na kuwaeleza juu ya hujuma hizo ili wazitambue.




