Madhara ya mvua kubwa mjini Dar es Salaam ...
| Madhara ya mvua kubwa mjini Dar es Salaam |
Leo imekuwa siku ngumu sana kwa uchukuzi mjini Dar es Salaam, Tanzania.
Kisa na maana,,,,mafuriko.| Wenyeji walitatazikika kuendesha shughuli zao za kawaida |
Baadhi ya barabara kuu za kitovu hicho cha kibiashara cha Tanzania, zilikuwa hazipitiki.
| maji kila maali |
Magari ambayo yalijaribu kutumia mabarabara ya Dar es Salaam yalikwama mengine huku yale yenye kimo cha juu yakifaulu kupita.
| Magari mengi yamekwama barabarani |
Mtangazaji wetu wa Dar es Salaam Sammy Awami amefaulu kuondoka nyumbani kwake na katika pita pita zake ametutumia picha hizi zinazoonesha hali halisia ya baadhi ya mabarabara ya Dar es Salaam.
| Wenye magari mjini Nairobi wataabika mabarabarani |
Barabara ya kisasa ya Thika Super Highway haipitiki baada ya mvuo kubwa kunyesha mchana na kusababisha mafuriko makubwa.
| Mtabiri wa hali ya hewa anasema mvua bado inatarajiwa |
Kinaya ni kuwa mtabiri wa hali ya hewa anasema kuwa mvua kubwa inatarajiwa kunyesa mjini Nairobi na maeneo mengi ya nchi.
Wenyeji wa mji huo wa Nairobi wameanza kutoa hasira zao kwenye mitandao ya kijamii wengi wakipiga picha maeneo yaliyokumbwa na mafuriko



