http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Mabalozi watatu wakabidhi hati za utambulisho kwa Rais

DK JOHN MAGUFULI RAIS John Magufuli amepokea hati za utambulisho za mabalozi watatu wanaoziwakilisha nchini zao hapa nchini. Balozi wa ...

DK JOHN MAGUFULI
RAIS John Magufuli amepokea hati za utambulisho za mabalozi watatu wanaoziwakilisha nchini zao hapa nchini. Balozi wa kwanza kukabidhi hati zake za utambulisho ni Carlos Alfonso Puente wa Brazil aliyesema kuwa nchi yake ipo tayari kuimarisha zaidi uhusiano na Tanzania.

Alitaja maeneo ya uzalishaji wa pamba na miwa kuwa ni miongoni mwa yatakayozingatiwa. Kwa upande wake, Rais Magufuli amemhakikishia Balozi Puente kuwa, Serikali itaendelea kushirikiana na nchi yake.

Pia alitaka uwekezaji na biashara kati ya Tanzania na Brazil uimarishwe zaidi, hasa ikizingatiwa kuwa Tanzania inazo rasilimali na fursa nyingi zinazoweza kutumika kwa faida ya pande zote mbili.

Mwingine aliyekabidhi hati zake za utambulisho ni Balozi Pavel Rezac wa Jamhuri ya Czech. Magufuli ameialika Czech kuungana na Tanzania katika juhudi zake za kuendeleza kilimo na kuzalisha umeme kwa kutumia gesi, ambayo mpaka sasa Tanzania imefanikiwa kugundua uwepo wa futi za ujazo zaidi ya trilioni 57.

Rais Magufuli alimuomba Balozi Rezac kumpelekea salamu Rais wa nchi hiyo, Milos Zeman, kumhakikishia kuwa Serikali yake ya Awamu ya Tano ipo tayari kuimarisha zaidi ushirikiano kukuza biashara na uwekezaji na kujenga uhusiano imara zaidi.

Balozi mwingine aliyewasilisha hati ya utambulisho ni Mariano Deng Ngor wa Sudani Kusini ambaye aliwasilisha salamu za Salva Kiir. Alisema, nchi hiyo itaendeleza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano wake na Tanzania.

Aliongeza kuwa, wanaheshimu mchango mkubwa unaotolewa na Tanzania katika kutatua mgogoro wa kisiasa nchini mwao. Rais Magufuli alisema, ataendeleza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kihistoria kati yake na Sudan Kusini.

Alitoa mwito kwa taifa hilo changa kufanya biashara moja kwa moja na Tanzania na nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambazo sasa idadi ya watu wake imefikia milioni 165.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli aliagana na Mahadhi Juma Maalim ambaye hivi karibuni alimteua kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait. Balozi Mahadhi anakwenda kuanzisha Ofisi za Ubalozi nchini Kuwait, ikiwa ni moja ya juhudi za Tanzania kuimarisha na kuongeza ushirikiano na uhusiano wake na nchi hiyo ya Mashariki ya Kati.

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Mabalozi watatu wakabidhi hati za utambulisho kwa Rais
Mabalozi watatu wakabidhi hati za utambulisho kwa Rais
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgPUmUd6PTPj2T3zJUFoxL7qhocsw3Se3mhpk906WDyHw6b4PwvgyPdTvxtUPXxQ3I0hUGH1_qZaykmjtXD1ImG-7xOd86iibstWtyAZWh3OvskGiAOc2N4lNEJfcm0XkUVcGBGaIlix0VB/s320/rais-magufuli1_210_120.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgPUmUd6PTPj2T3zJUFoxL7qhocsw3Se3mhpk906WDyHw6b4PwvgyPdTvxtUPXxQ3I0hUGH1_qZaykmjtXD1ImG-7xOd86iibstWtyAZWh3OvskGiAOc2N4lNEJfcm0XkUVcGBGaIlix0VB/s72-c/rais-magufuli1_210_120.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/04/mabalozi-watatu-wakabidhi-hati-za.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/04/mabalozi-watatu-wakabidhi-hati-za.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy