http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Kigogo TBC ‘ajimilikishia’ kiwanja cha shirika

NAIBU WAZIRI WA HABARI,UTAMADUNI,SANAA NA MICHEZO.ANASTAZIA WAMBURA NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wamb...

NAIBU WAZIRI WA HABARI,UTAMADUNI,SANAA NA MICHEZO.ANASTAZIA WAMBURA
NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura, ametoa siku saba kwa Meneja Rasilimali Watu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Neema Mrindoko kujieleza sababu za kuandika jina lake katika kiwanja cha shirika kilichopo Kisarawe mkoani Pwani.

Wambura alitoa agizo hilo juzi alipotembelea kiwanja hicho kilichopo eneo la Kimani ambacho mpaka sasa hakijakamilisha usajili wake na kupewa hati wakati kilinunuliwa na shirika hilo mwaka 2012. Kiwanja hicho kimejengwa nyumba za watumishi ambao wangekuwa wakifanya kazi katika kituo cha Kisarawe lakini hazijakamilika.

“Natoa siku saba, mtu huyu awe amenipa maelezo ya kutosha kwa nini hati hiyo imesainiwa na mtu mmoja ambaye ni yeye na ameandika jina lake badala ya jina la Shirika, ina maana alikuwa hajui? Hii ni makusudi,” alisema Wambura.

Wambura alisema mtu huyo amefanya makusudi kwa nafasi yake kushindwa kutambua kukaa miaka yote hiyo bila kupewa hati na kutelekezwa bila kuendelezwa ni ufisadi ambao hauwezi kuvumiliwa.
Awali Wambura alipokuwa akipokea taarifa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya hiyo, Mwanamvua Mrindoko, alisema kiwanja hicho chenye meta za mraba 9,567 kilipimwa na kusajiliwa kwa namba 68,480 mwaka huo huo shirika liliomba kuandaliwa hati.

Mrindoko alisema utaratibu wa ukamilishaji hati ulifanyika na walilipia na kujaza fomu ya maombi ya hati. Ilielezwa kwamba, baada ya TBC kuisaini na kuirudisha Wizara ya Ardhi ilionekana kuwa na upungufu ikarudishwa.
Alitaja upungufu huo kuwa ni hakukuwa na nakala halisi ya kuanzishwa shirika na pia fomu hiyo ilisainiwa na mtu mmoja badala ya wahusika wawili wa TBC na hivyo kukwamisha mchakato wa kupata hati.

Naibu Waziri huyo alipomhoji Ofisa miradi wa wizara hiyo, Macksselin Chota ambaye alikuwepo kwenye ziara, alisema maelezo hayo ni sahihi na kwamba upungufu wanaufanyia kazi. Chota alisema viwanja vingi vya TBC havijapata hati.

Kati ya viwanja 55, viwanja 19 pekee ndivyo vyenye hati. Alisema pia viwanja vingi viko katika migogoro mbalimbali kama vile uvamizi na pia uporaji. Naibu Waziri Wambura aliagiza ndani ya siku hizo saba hati ya kiwanja hicho cha Kisarawe iwe imepatikana.

Alitaka shirika pia lieleze ni namna gani watafanya kuendeleza majengo ambayo yameanza kujengwa hapo. “Hii inatia mashaka kabisa, mnachelewesha kupata hati na baadaye viwanja vinaingia kwenye migogoro, unafanya hivyo ili baadaye nyie wenyewe mzunguke, tutashindwaje kuamini hivyo?” Alihoji Naibu Waziri

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Kigogo TBC ‘ajimilikishia’ kiwanja cha shirika
Kigogo TBC ‘ajimilikishia’ kiwanja cha shirika
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgol91E5boy4LSuGfTdRqO5SAG7HSMdr4eE83SIsmDns9iHEfMJnF8sdM_ECh72sv1DJPHlX5EIVJ-hP1vElF2OdQ7R8pfXlUFD5a23_2hz67TWkuJI55ziTXZNKzjHGvneSMWPNllPUaUY/s320/anastazia-wambura_210_120.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgol91E5boy4LSuGfTdRqO5SAG7HSMdr4eE83SIsmDns9iHEfMJnF8sdM_ECh72sv1DJPHlX5EIVJ-hP1vElF2OdQ7R8pfXlUFD5a23_2hz67TWkuJI55ziTXZNKzjHGvneSMWPNllPUaUY/s72-c/anastazia-wambura_210_120.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/04/kigogo-tbc-ajimilikishia-kiwanja-cha.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/04/kigogo-tbc-ajimilikishia-kiwanja-cha.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy