Askofu Josephat Gwajima KESI ya kushindwa kuhifadhi silaha kwa usalama inayomkabili Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwaji...
![]() |
| Askofu Josephat Gwajima |
Kesi hiyo ilitajwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Cyprian Mkeha kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa lakini iliahirishwa kwa kuwa shahidi wa upande wa Jamhuri hakufika mahakamani.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Shadrack Kimaro aliomba iahirishwe kwa kuwa shahidi aliyetakiwa kutoa ushahidi, hakufika mahakamani kutokana na kufiwa. Hakimu Mkeha aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 2 mwaka huu.
Mbali na Gwajima, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni msaidizi wa askofu huyo, Yekonia Bihagaze (39), mfanyabiashara George Mzava (43) , na mkazi wa Kimara Baruti, Geofrey Milulu (31).
Inadaiwa kuwa, Machi 29 mwaka jana, katika Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni A, washtakiwa walikutwa wakimiliki bastola aina ya Baretta yenye namba CAT 8802 bila kuwa na kibali kutoka mamlaka inayohusika na silaha na milipuko.
Aidha, inadaiwa washtakiwa hao walikuwa wakimiliki isivyo halali risasi tatu za bastola pamoja na risasi 17 za bunduki aina ya shotgun. Gwajima anadaiwa kushindwa kuhifadhi silaha katika hali ya usalama.




