Jenerali Athanase Kararuza wakati mmoja alihudumu kama kamanda wa vikosi vya AU nchini CAR Afisa mkuu wa jeshi la Burun...
![]() |
| Jenerali Athanase Kararuza wakati mmoja alihudumu kama kamanda wa vikosi vya AU nchini CAR |
Afisa mkuu wa jeshi la Burundi ameuawa pamoja na mkewe baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana mjini Bujumbura.
Wizara ya ulinzi imethibitisha kifo chake.
Jenerali huyo ndiye afisa wa karibuni zaidi wa jeshi kuuawa katika mji huo mkuu wa Burundi tangu kufanyika kwa jaribio la kupindua serikali ya Rais Pierre Nkurunziza mwaka jana.




