Serikali hapa Nchini imewataka wananchi kutoa taarifa pale watakapobaini uwepo wa viashiria vya uhalifu ikiwemo ubakaji, mauaji au utekaji...
Serikali hapa Nchini imewataka wananchi kutoa taarifa pale watakapobaini uwepo wa viashiria vya uhalifu ikiwemo ubakaji, mauaji au utekaji Ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria na vitendo hivyo kukomeshwa.
Hayo yameelezwa Oct 7, 2024 na Naibu waziri wa mambo ya ndani ambae pia ni Mbunge wa jimbo la Babati Vijijini Daniel Sillo ambae amekuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kidato Cha nne Shule ya Sekondari Matufa iliyoko Kata ya Magugu Wilaya Babati mkoani Manyara.
Hata hivyo Sillo amelaani vikali tukio la Mwanamke wa
Kata ya Magugu ambae ameuwawa Kwa kubakwa na kulawitiwa ambapo ameitaka jamii
kukemea vitendo hivyo vya kikatili na kuitaka jamii kuwalea watoto wao kwa
kuzingatia maadili.
Kwa upande wake mkuu wa shule ya Sekondari Matufa Herin Mfwangavo, amesema Shule yake imekuwa ikifaulisha wanafunzi kila mwaka huku akimuomba Mbunge huyo kutatua changamoto zinazoikabili Shule hiyo ikiwemo ya kutokuwa na maji katika vyoo vya wanafunzi na Walimu.
Akisoma risala Kwa niaba ya wahitimu wa darasa la Saba
mmoja wa wanafunzi hao Nusura Majid amesema shule hiyo pia inakabiliwa na
changamoto ya upungufu wa madarasa na madawati ambapo mgeni rasmi amekabidhi
zawadi ya mashine ya kutolea nakala Kwa shule hiyo (Photocopy mashine)