Halmashauri ya Wilaya ya Igunga imekabidhiwa mifuko mia moja ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati za kujifungulia kina m...
Halmashauri ya Wilaya ya Igunga imekabidhiwa mifuko mia moja ya saruji
kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati za kujifungulia kina mama ili kuepusha
vifo vya mama na mtoto.
Msaada
huo umetolewa na Mheshimiwa Munde Tambwe Mbunge wa viti maalumu wa Chama
cha mapinduzi mkoa wa Tabora alipokuwa katika mapokezi ya Mwenyekiti wa
Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Ndugu Gaudentia Mugossi Kabaka
Wilayani Igunga mkoani Tabora.
Akikabidhi
msaada huo Mheshimiwa Tambwe alisema Ukosefu wa Zahanati na vituo vya
afya vya kujifungulia akina mama wajawazito imekuwa ni sababu kuu ya
vifo vya kina mama na watoto wachanga na kupunguza nguvu kazi ya Taifa.
Mheshimiwa
Tambwe alitoa mchanganuo wa mifuko hiyo ya saruji kuwa kila jimbo la
Halmashauri ya Wilaya ya Igunga kupatiwa mifuko hamsini ya saruji na
kuitumia katika ujenzi wa Zahanati na vituo vya afya watakavyopanga wao.
Akipokea
msaada huo, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wikaya ya Igunga
Ndugu Revocatus Kuuli alimshukuru Mheshimiwa Tambwe na kuahidi kugawa
mifuko hiyo kwa Wabunge wa majimbo ya Igunga na Manonga.
Ndugu
Kuuli aliwaomba viongozi wa Chama na Serikali kuendelea kuwakumbuka
wanawake maana ndiyo jeshi kubwa la wapiga kura wao ikilinganishwa na
wanaume na vijana wanaojitokeza kupiga kura katika chaguzi mbalimbali.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Igunga Ndugu John Mwaipopo aliwaomba wanawake wa
Chama cha Mapinduzi Igunga kuiga mfano wa viongozi wanawake katika
serikali na vyama na pia kumshukuru Mheshimiwa Munde Tambwe.
Msaada
huo wa ujenzi wa Zahanati na kituo cha afya uliambatana na Mchango wa
vikundi vya wanawake wajasiriamali wa Shilingi Laki tano uliokuwa ni
ahadi ya Mheshimiwa Munde Tambwe.
Akizungumza
kwa niaba ya Kikundi hicho, Mwenyekiti wao Mama Agatha alimuahidi
Mheshimiwa Tambwe kuwa watakuwa nae pamoja kuhakikisha maendeleo ya
Wanawake yanapatikana.
Michango
hii imeambatana na uzinduzi wa vibanda vya biashara vinavyomilikiwa na
Umoja wa Wanawake Tanzania wilaya Igunga chini ya udhamini wa Mheshimiwa
Munde Tambwe.
Ikumbukwe
kuwa Umoja wa Wanawake Tanzania ni moja ya Jumuiya zilizopo chini ya
Chama cha Mapinduzi ukiwa pamoja na Jumuiya ya Wazazi Tanzania na Umoja
wa vijana CCM (UVCCM).
Habari na Nassor Amour, Igunga