NA Nassor Amour Mwili wa aliyekuwa mzazi mwenzie na Mwanamuziki wa kizazi kipya na mjasiriamali Zuwena Mohamed a...
Nassor Amour |
![]() |
Mwili wa aliyekuwa mzazi mwenzie na Mwanamuziki wa kizazi kipya na mjasiriamali Zuwena Mohamed almaarufu Shilole ukiwekwa ndani ya kaburi |
![]() |
wafanyakazi wenzake aliyekuwa mzazi mwenzie na Mwanamuziki wa kizazi kipya na mjasiriamali Zuwena Mohamed almaarufu Shilole wakiweka mashada ya maua katika kaburi |
Bwana Makala Jofrey Joseph alizaliwa tarehe 28/02/1980 na alifariki mnamo tarehe tano mwezi wa sita mwaka huu majira ya saa nane usiku kwa mauti kumfika ghafla akiwa amelala nje ya nyumba yake alipokuwa akiishi pamoja na mkewe na mtoto wao mmoja aliefahamika kwa jina la Moshi Makala.
Akizungumza na wanahabari nyumbani kwao, Mdogo wa Marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Paul Jofrey Joseph ambae pia ni muimbaji wa muziki wa kizazi kipya wilayani Igunga amesema, Marehemu alikutwa akiwa amelala nje ya chumba chake kama kawaida yake akiwa ametoka kazini hujipumzisha mahali hapo.
Aidha amesema, Marehemu ameacha mjane mmoja na watoto wawili ambao ni Moshi Makala na Joyce Makala (Mtoto wa Shilole) ambao wote alikuwa akiwahudumia mwenyewe akishirikiana na familia yake iliyopo Igunga mjini.
Pia ameeleza uhusiano wa Marehemu Makala na Msanii Shilole ulikuwepo japo ulikuwa ni wa huduma za mtoto tu na si kimapenzi kama baadhi ya watu walivyozusha na pia kukanusha tetesi za ubakaji uliofanywa na marehemu dhidi ya Msanii huyo.
Kwa upande wake msanii Shilole alikataa kuongea na wanahabari kwa madai ya kutokuwa na muda huo kwani bado ana mambo ya kifamilia anaongea na wanafamilia wake hivyo kufanya jitihada za kuzungumza nae kugonga mwamba.

Lakini pia wanahabari hawakupata fursa ya kuongea na watoto na baadhi ya ndugu wa marehemu kutokana hali halisi ya majonzi waliokuwa nayo kwa muda wote wa msiba.
Makala Jofrey ni mtoto wa pili kati ya watoto wane wa mama mmoja katika Familia ya Mzee Jofrey Joseph ambapo ameacha dada yake mmoja na wadogo zake wawili pamoja na ndugu waliochangia mzazi mmoja mmoja.

Msiba wa Makala Jofrey Joseph ulihudhuriwa na wanahabari mbalimbali, wasanii wa kizazi kipya na maigizo kutoka Igunga, Viongozi wa Vyama na Serikali na vijana pamoja na wazee maarufu wa mji wa Igunga.
