Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu kwa jina la Mzee wa Upako, amemtaja msanii ambaye anamkubali kati ya Al...

Mchungaji
wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu kwa jina la Mzee
wa Upako, amemtaja msanii ambaye anamkubali kati ya Alikiba na Diamond
pamoja na kutoa sababu zake.
Akiongea
na kipindi cha Maisha Mseto cha Times FM, Mzee huyo wa Upako amesema
anampenda sana Diamond kwa sababu ni mnyenyekevu lakini Alikiba ni
kiburi.
“Mimi
nampenda sana Diamond kwa sababu ni mnyenyekevu, Simpendi Alikiba kwa
sababu ana kiburi, nadhani kwa sababu amekaa Kariakoo,” amesema
Lusekelo.
Mchungaji
huyo ameongeza kwa kusema, “Ukipigia simu Diamond anapokea kwa
unyenyekevu ila Alikiba anapokea kwa maringo. Ndio maana Diamond amefika
mbali.”



