http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

SERENGETI BOYS YAIFUNGA DYNAMO, KUTUA USIKU WA MANANE

Timu ya Mpira wa Miguu ya vijana wa Tanzania wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imefanya kambi yake kwa mafanikio huko jijini ...




Timu ya Mpira wa Miguu ya vijana wa Tanzania wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imefanya kambi yake kwa mafanikio huko jijini Victoria kwenye Kisiwa cha Mahe, nchini Shelisheli baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya dhidi ya Northern Dynamo.

Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Taifa wa Shelisheli, bao pekee la Serengeti Boys lilifungwa na Muhsin Makame katika dakika 75 ya mchezo huo uliokuwa na ushindani mkali katika vipindi vyote viwili kutokana na kushambuliaana mara kwa mara.

Serengeti Boys ambayo ilikuwa na kikosi cha nyota 21 na viongozi watano, wamemaliza kambi ya huko Shelisheli na hivyo inaondoka jioni ya leo Septemba 13, 2016 saa 11:00 jioni na ikitarajiwa kuingia nchini usiku wa saa 7:45 Septemba 14, 2016 ambako itakuwa kambini hadi siku ya mchezo Jumapili Septemba 18, mwaka huu.

Mchezo huo wa kuwania kucheza fainali za kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17. Fainali hizo zitafanyika jijini Antananarivo, Madagascar hapo Aprili, 2017.

Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Nyundo Shime maarufu kwa jina la Mchawi Mweusi, amesema: “Sitaki kuwa na maneno mengi. Nataka Watanzania waje kuona wenyewe. Maana maneno maneno yakizidi inakuwa kama kero. Nataka kujenga utamaduni wa Watanzania kuja wenyewe uwanjani kuona timu yao.”

Katika hatua nyingine, wapinzani wa Serengeti Boys wanatarajiwa kutua Alhamisi wakiwa na kikosi cha watu 40 na kati ya hao ni 22 ni wachezaji. Miongoni kwa kundi hilo pia kuna wanahabari wanne.

Katika orodha ilitumwa TFF, wachezaji wa timu hiyo ni pamoja na Mathieu Lee Valtair, Balou Prince Joel, Bopoumela Chardon, Kiba Konde Ridrique, Kibasila Christ Benilde, Langa Lessen Bercy, Makouana Beni, Mantouari Juste Aldo, Mata Thomas, Mbemba Patchely Rael, Mbenza Kamboleke, Mboungou Prestige, Mebeza Egouep Craiche, Mouandza Mapata, Moungala Ikounga, Mountou Edouard, Ngakosso oko Alves, Ngaloukossi Jossy Ronel, Nguienda Mouanga Bernice, Nguimbi Exau, Ntoto Gedeon, Oboua Danish na Otang Jeordon.

Viongozi wa timu hiyo wamo Ntoto Lacombe ambaye ndiye Mkuu wa Msafara, Goma Ambroise Stephane ambaye ni Mratibu wa msafara, Ngami Gobard – Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Congo – Brazzavile.

Wengine ni maofisa mbalimbali Otende Charles, Moussavou Merrile, Badji Mombo, Berrettini Paulo, Ekariki Basile, Cesana Eraldo, Bakoua Loufouma Narcisse, Okandze Elenga Jean Pierre, Lounou Joste Feller, Mabila Kengue Francois, Loemba Jean Rufin, Mendome Ndoum, Batangounna Ntari na Mbemba Gervais.

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : SERENGETI BOYS YAIFUNGA DYNAMO, KUTUA USIKU WA MANANE
SERENGETI BOYS YAIFUNGA DYNAMO, KUTUA USIKU WA MANANE
http://fullshangweblog.com/home/wp-content/uploads/2016/09/Under15.png
WEPESI MEDIA
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/09/serengeti-boys-yaifunga-dynamo-kutua.html
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/09/serengeti-boys-yaifunga-dynamo-kutua.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy