Wana kijiji watano katika eneo lililokumbwa na ukame kaskazini mwa India wamefariki wakijaribu kutafuta maji katika kisima kisichotum...
Wana kijiji watano katika eneo
lililokumbwa na ukame kaskazini mwa India wamefariki wakijaribu kutafuta
maji katika kisima kisichotumika.
Eneo kubwa la India linakabiliwa na ukame mbaya ambao umewaua takriban watu 300.
Haryana na majimbo mengine wiki iliopita yalikosolewa na mahakama ya juu nchini India kwa kushindwa kutambua tatizo hilo la maji.
Uhaba wa maji india |
Ripoti katika eneo hilo zinasema kuwa wanaume hao kutoka wilaya ya Jindi huko Haryana waliamua kujaribu kukitengeza kisima hicho ili kuweza kukabiliana na ukosefu wa maji katika eneo hilo.
Lakini naibu afisa wa polisi katika wilya hiyo Virender Singh alikana kwamba walihitaji maji ya kunywa akisema wanaume hao walitaka kukitumia kisima hicho kwa maji ya kuoga na kuosha.
''Kisima hicho kilikuwa hakijatumika kwa takriban miaka mitano hadi sita na gesi yenye sumu ilikuwa imetanda huko chini'',aliambia kituo cha habari cha AFP